Local,Normal News,

CHAN 2025 yapigwa kalenda hadi August 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Jan 2025
CHAN 2025 yapigwa kalenda hadi August 2025

Shirikisho la Soka barani Afrika CAF limetangaza kuisogeza mbele michuano ya mataifa bingwa ya Afrika CHAN hadi Agosti mwaka huu

Taarifa ya shirikisho hilo imebainisha kwamba wameahirisha michuano hiyo licha ya waandaaji ambao ni Kenya, Tanzania na Uganda kufanya vema katika maboresho ya viwanja, hoteli, hospitali na miundombinu na vifaa vingine kwa ajili ya kuandaa michuano hiyo

Hata hivyo wataalam wa Ufundi na Miundombinu wa CAF ambao baadhi yao wapo kwenye nchi hizo za Afrika Mashariki wamelishauri shirikisho hilo kuwa muda zaidi unahitajika kuhakikisha miundombinu na vifaa vipo kwenye viwango vinavyohitajika zaidi ili michuano hiyo ifanikiwe ipasavyo

Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe amewashukuru Marais William Ruto wa Kenya, Dk Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea na maendeleo mazuri yaliyofikiwa hasa kwenye ujenzi wa miundombinu

Licha ya michuano hiyo kusogezwa mbele shughuli ya upangaji wa ratiba ya michuano hiyo itafanyika kesho kuanzia saa 2:00 usiku Mjini Nairob, Kenya lakini tarehe rasmi ya kuanza michuano hiyo itatajwa baadae

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
30m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’