Local,Normal News,Yanga

Kamwe atoa tahadhari kuikabili MC Alger

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Jan 2025
Kamwe atoa tahadhari kuikabili MC Alger

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema mechi dhidi ya MC Alger ni ngumu hivyo wanapaswa kuendea mchezo huo kwa tahadhari kubwa

Kamwe amesema mijadala mingi inayoendeshwa huko mitandaoni inaonesha kama Yanga inakwenda kushinda kirahisi na kutinga robo fainali lakini sivyo

"Tumeona mijadala mbalimbali katika magrupu ya Whatsapp, inaonekana mashabiki wa Yanga wanaona kama mchezo dhidi ya MC Alger ni mwepesi na tunaenda kumpiga mwarabu kirahisi"

"Lakini niwaambie mechi hii ni ngumu sana tunapaswa tujiandae sawa sawa na tujitokeze kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuwapa hamasa wachezaji wetu"

"wakati tunacheza mchezo wa fainali kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger, tuliamini mechi ya hapa nyumbani ingekuwa nyepesi na tungeshinda kirahisi"

"Wapinzani wetu wakatumia kujiamini kwetu kulikopitiliza na kutuadhibu hapa nyumbani hivyo hatupaswi kurudia makosa"

"Yanga inawahitaji mashabiki 60,000 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi. Itakuwa ni aibu kama tutashindwa kutumia nafasi yetu nyumbani kujaza uwanja"

"Ni jukumu la kila shabiki na mwanachama wa Yanga kwenda vituoni kukata tiketi lakini pia ni jukumu la kila Mwanayanga kushiriki kuiombea dua timu yetu ili iweze kushinda mchezo huo," alisema Kamwe

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’