Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha kumsajili mshambuliaji raia wa Ghana Jonathan Sowah
Sowah tayari ametua Singida BS sambamba na Mghana mwenzie, Frank Assinki anayecheza nafasi ya beki wa kati
Hivi karibuni Singida BS ilitangaza kuachana na mshambuliaji raia wa Ivory Coasta Joseph Guede ambaye nafasi yake sasa inajazwa na Sowah
Unaweza kusema katika dirisha dogo la usajili lililofungwa juzi, Singida BS ilishusha 'vyuma' kwelikweli
Jana Singida BS ilithibitisha kumnasa winga raia wa Ivory Coast Serge Pokou aliyekuwa akiitumikia Al Hilal ya Sudan
Singida Black Stars pia imethibitisha kumsajili kipa Amas Obasogie kutoka nchini Nigeria
Obasogie anajiunga na klabu hiyo ya mkoani Singida akitokea Fasil Kenema SC ya Ethiopia