Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Januari 23 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Jan 2025
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Januari 23 2025

Wawakilishi wa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford walikutana na viongozi wa Barcelona siku ya Jumanne huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akitafuta njia ya kuondoka Manchester United. (Sky Sports)

Arsenal inamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Slovenia na klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani Benjamin Sesko, 21. (Sportsport)

AC Milan imefikia mkataba wa kumsajili beki wa Uingereza Kyle Walker, 34, kutoka Manchester City ambao utakuwa mkopo wa awali lakini unajumuisha chaguo la kununua kwa euro 5m (£4.2m). (Sky Sports Italia)

Winga wa Manchester United Alejandro Garnacho anapendelea kuhamia Chelsea badala ya Napoli, ambako ombi lao la kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 limekataliwa. (TyC Sports, kupitia Metro)

Napoli pia inpania kumsajili winga wa Ujerumani Karim Adeyemi, 23, kutoka Borussia Dortmund. (Fabrizio Romano)

Wachezaji watatu wa Chelsea huenda wakakihama klabu hicho mwezi huu huku mlinzi wa Ureno Renato Veiga, 21, akishinikiza kuungana na Juventus (Mail)

Nottingham Forest inaandaa dau la kubbwa ambalo huenda likafikia pauni milioni 60, ili kumsajili mshambuliaji wa Brazil Matheus Cunha, 25, kutoka Wolves. (Sky Sports)

Juventus wameipa Chelsea fursa ya kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, ambaye pia ananyatiwa na Manchester City na Arsenal. (TeamTalk)

Kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 31, anazingatia ofa kadhaa kutoka kwa timu za ligi tano kuu za Ulaya, lakini makubaliano ya mkataba hayajafikiwa. (ESPN)

Mustakabali wa mkurugenzi wa ufundi wa West Ham Tim Steidten katika klabu hiyo uko mashakani baada ya The Hammers kukamilisha dili la kumsajili mchambuzi wa masuala ya uajiri wa Chelsea Kyle Macaulay, ambaye amewahi kufanya kazi na kocha Graham Potter. (Guardian)

Everton wameonyesha nia ya kumsajili winga wa Sporting Muingereza Marcus Edwards, 26. (kutoka Caught offside)

Wakala wa Emerson Royal wa AC Milan, 26, amezungumza na Everton na Fulham, lakini beki huyo wa Brazil pia analengwa na Galatasaray. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Manchester United wanatathmini iwapo watawasilisha dau lililoboreshwa la kumnunua beki wa Lecce Patrick Dorgu baada ya ombi la awali la mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark kukataliwa. (Star)

Lakini Napoli wanatumai kuipiku Manchester United kupata saini ya Dorgu. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
7m ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
59m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’