Simba imesonga mbele kibabe kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kuifumua Kilimanjaro Wonders mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Unaweza kusema ilikuwa ni suala la mabao mangapi Simba itafunga katika mchezo huo ambao ulitofautishwa na ubora wa wachezaji wa Simba dhidi ya vijana wa Kili Wonders
Mabao manne yalfungwa kipindi cha kwanza yakiwekwa kambani na Valentine Mashaka, Ladark Chasambi na Joshua Mutale huku Patrick Sebastian akijifunga
Steven Mukwala na Edwin Balua wakafunga kalamu ya mabao katika kipindi cha pili na kufanya ubao usome 6-0