Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Januari 28 2025

Joel JJ By Joel JJ β€’ 28th January 2025


Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne Januari 28 2025

Manchester United huenda ikamnunua mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Christopher Nkunku, 27, kwa mkopo ikiwa Muingereza Marcus Rashford, 27, ataondoka katika klabu hiyo. (The Athletic – Subscription Required)

Mshambuliaji Rashford yuko tayari kusubiri kupata uhamisho wa kwenda Barcelona. (Mirror) Bayer Leverkusen wamefanya mawasiliano na Manchester City kuhusu uhamisho wa mkopo wa kiungo wa kati wa England chini ya umri wa miaka 21 James McAtee, 22. (Daily Mail)

Kocha wa City Pep Guardiola hatamzuia Mctee iwapo anataka kujiunga na mabingwa hao wa Ujerumani. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Argentina Emiliano Buendia, 28, yuko mbioni kujiunga na Leverkusen kutoka Aston Villa kwa mkopo. (Florian Plettenberg)

Villa pia wako kwenye mazungumzo na mlinzi wa Villarreal mwenye umri wa miaka 27 na Argentina Juan Foyth. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Villa na Colombia Jhon Duran, 21, analengwa na klabu ya Saudi Arabia Al-Nassr kwa euro 100m wakati wanatafuta mshirika mpya wa Cristiano Ronaldo. (Football Transfers)

Wolves wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Lens na Austria yenye thamani ya £16m Kevin Danso, 26. (Telegraph - subscription required)

Liverpool na Chelsea wako tayari kuchuana na Napoli kwa ajili ya kumnunua fowadi wa Borussia Dortmund na Ujerumani Karim Adeyemi, 23, lakini wanaweza kusubiri hadi msimu wa joto kufanya uhamisho. (Corriere Dello Sport – In Itali)

Real Madrid, Bayern Munich na Juventus wanavutiwa na beki wa kimataifa wa Bournemouth chini ya umri wa miaka 21 Dean Huijsen. (Fichajes – In Spanish)

Newcastle wanavutiwa na mlinzi wa kimataifa wa Ukraine wa Cherries, Illia Zabarnyi, 22, lakini wanajua kuwa dili halitawezekana hadi msimu wa joto. (i Paper)

Aston Villa wamekubali makubaliano ya kibinafsi na beki wa Chelsea na Ufaransa Axel Disasi, 26. (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ureno Joao Felix, 25, pia anavutiwa na Aston Villa lakini wangeweza tu kuchukua mchezaji mmoja kwa mkopo kutoka Stamford Bridge. (Sportsport)

Mshambulizi wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, anatarajiwa kuondoka Brighton kwa mkopo kabla ya mwisho wa dirisha la uhamisho. (Fabrizio Romano)

Ferguson ndiye anayelengwa na kocha wa zamani wa Seagulls, Graham Potter, ambaye anataka kumleta mshambuliaji huyo West Ham, lakini Everton, Bournemouth na Arsenal pia wamo mbioni. (Sportsport)

Chelsea wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 21, na mshambuliaji wa Bayern Munich na Ufaransa Mathys Tel, 19, baada ya kuamua kwamba kuwaongezea mshambuliaji ni muhimu kuliko kuongeza safu ya ulinzi Januari. (TeamTalk)

Brentford wanafikiria kumnunua mlinzi wa zamani wa Chelsea Andreas Christensen, 28, lakini raia huyo wa Denmark anataka kupigania nafasi yake Barcelona. (Independence)

Kiungo wa kati wa Chelsea na Italia Cesare Casadei, 22, anatazamiwa kujiunga na Lazio kwa mkataba wa kudumu wa pauni milioni 11. (90min)

Wolves na Leicester wanavutiwa na kiungo wa kati wa Uingereza Alex Oxlade-Chamberlain, 31, ambaye kwa sasa anachezea Besiktas. (Sun)

St Johnstone wamekataa ofa mbili kutoka kwa Fulham za kumnunua mshambuliaji wa Scotland Brodie Dair, 16. (The Courier)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.