Local,Transfer News,Yanga

Maxi apuuza tetesi kucheza kwa mkopo Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Jan 2025
Maxi apuuza tetesi kucheza kwa mkopo Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli amesema hana muda wa kufuatilia yanayozushwa kuhusu mkataba wake na Yanga kwani hilo sio jukumu lake

Akiwa katika msimu wake wa pili na Yanga, tayari tetesi zimeanza kuhusu hatma yake baadhi ya taarifa zikidai hatasaini mkataba mpya huku wengine wakidai mchezaji huyo anaitumikia Yanga kwa mkopo kutoka AS Maniema

Imekuwa ni kawaida kwa wachezaji wa DR Congo wanaoitumikia Yanga kuzushiwa kuwa wanacheza kwa mkopo. Ilikuwa hivyo kwa mshambuliaji wa zamani wa mabingwa hao wa nchi Fiston Mayele ambaye kwa sasa anaitumikia Pyramids Fc

Maxi amesisitiza yeye ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kutimiza majukumu yake kama mwajiriwa wa Yanga

"Kwanza niseme wazi, mimi sihusiki na tetesi, hayo ni mambo yenu nyie Wanahabari ili muuze habari"

"Pili mimi nafanya kazi yangu kama mwajiriwa wa Yanga. Kama niko hapa kwa mkopo mimi silijui hilo na wala sitaki kujua nilinunuliwa pia sijui"

"Niulize swali kuhusu majukumu yangu ndani ya Yanga, Kitu kikubwa ninachokiwaza je kocha atanipa nafasi Jumamosi niweze kuitetea nembo ya mwajiri wangu Yanga? Niulize hilo swali," alisema Maxi

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga ni kuwa makubaliano ya kuhuisha mkataba wa Maxi yamefikiwa, ni suala la muda tu Yanga itatangaza kumuongeza mkataba mchezaji huyo kiraka

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’