Local,Transfer News,Yanga, Simba, Azam, Fountain Gate, Singida BS

Morocco ataka maandalizi kabambe Afcon 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Jan 2025
Morocco ataka maandalizi kabambe Afcon 2025

Ili kuhakikisha Timu ya Soka ya Taifa (Taifa Stars), inafanya vizuri katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), maandalizi yake yawe ni 'jambo' la kitaifa na si kuacha jukumu hilo kwa Serikali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeelezwa

Katika fainali hizo zitakazofanyika kuanzia Desemba 21, mwaka huu hadi Januari 18, mwakani nchini Morocco, Taifa Stars imepangwa Kundi C pamoja na Uganda (Cranes),Tunisia na Nigeria

Stars itatupa karata yake ya kwanza Desemba 23, mwaka huu kwa kuivaa Nigeria halafu Desemba 27 itakutana na 'majirani' zake Uganda na itamaliza mechi za hatua ya makundi Desemba 30 kwa kupambana na Tunisia kwenye Uwanja wa Prince Moulay ulioko jijini, Rabat

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Morocco' amesema ili kuweka rekodi ya kufanya vyema katika fainali hizo, maandalizi ya timu hiyo yanapaswa kuwa ni jukumu la kitaifa

Morocco amesema kipindi cha miezi 11 iliyobakia kabla ya kufanyika kwa fainali hizo, matokeo chanya yanaweza kupatikana kama tutaongeza ushirikiano kuanzia hatua ya kwanza

"Hili jambo si la mwalimu au benchi la ufundi, ni suala la kitaifa hasa pale katika uwezeshwaji wa kutekeleza mipango ya mwalimu, sisi kama benchi la ufundi tutakuja na programu yetu na naamini ikifuatwa vyema tutafanya vizuri kwenye fainali hizi," alisema Morocco

Kocha huyo alisema TFF inahitaji msaada ili kukamilisha programu za kiufundi za timu hiyo ambayo haijawahi kuvuka hatua ya makundi

Aliongeza kuwafahamu mapema wapinzani wao ni jambo zuri kwa sababu watapata muda mzuri wa kuwafuatilia na kujiandaa kuwakabili

"Mimi naamini tumepiga hatua kwenye makundi katika kutafuta nafasi ya kushiriki, tumefanya vizuri lakini haitoshi, tunahitaji kupambana zaidi na kuendeleza pale tulipofikia," alisema kocha huyo mwenye asili ya Zanzibar

Aliongeza katika fainali hizo hakuna timu nyepesi, kila timu iliyofuzu inaweza ikawa tishio, lakini hakuna nchi wanayoihofia

"Of course' timu zote ambazo zimefuzu ni tishio, kufika hatua ya fainali za AFCON si jambo la rahisi, la msingi ni kuhakikisha tunajipanga vizuri ili tuwe bora zaidi," Morocco aliongeza

Kabla ya kushiriki fainali hizo za AFCON, Taifa Stars imekata tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), zitakazofanyika kuanzia Agosti 2 hadi 30, mwaka huu

Tanzania, Kenya na Uganda ndio wenyeji wa fainali hizo za CHAN, ambazo awali zilitarajiwa kufanyika kuanzia mapema Februari, mwaka huu. Shirikisho la Soka Afrika (CAF), imezipa nchi hizo tatu wenyeji wa michuano ya CHAN ili kuwapa uzoefu kuelekea Fainali za AFCON za mwaka 2027 ambazo zitaandaliwa na mataifa hayo matatu ya Afrika Mashariki

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’