Local,Normal News,Yanga

Ramovic aihofia Kagera Sugar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Feb 2025
Ramovic aihofia Kagera Sugar

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema wamejiandaa kwa mechi ngumu ya ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambayo itapigwa leo Jumamosi katika uwanja wa KMC Complex

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari jana, Ramovic alisema Kagera Sugar ni timu ngumu na watahitaji kuwa bora katika mchezo huo ili kuibuka na ushindi

Ramovic alisema dhamira ya Yanga ni kushinda kila mchezo ili kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi, hivyo watapambana ili kushinda mchezo huo

"Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu hivyo tunapaswa kucheza vizuri zaidi na kiukweli tunawaheshimu sana Kagera Sugar, Tunajua watakuja vizuri hasa kwa Kujilinda zaidi hivyo tunapaswa kutumia nafasi tutakazozitengeneza"

"Lengo letu kubwa ni kupata alama tatu kesho, sisi tunatazama zaidi mechi zetu na tuna jukumu la kushinda kila mchezo ili kurudi kileleni, tunajua ubora wa Kagera Sugar hivyo tuna jukumu la kucheza kwenye ubora wetu wa kila siku"

"Tuna mechi 15 mbele yetu, tunakwenda kucheza dhidi ya timu shindani kama tulivyo sisi, tunahitaji kushinda mechi zetu pasipo kuangalia matokeo ya wengine ili kuwa mabingwa," alisema Ramovic

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, beki Nickson Kibabage alisema wanatambua mechi dhidi ya Kagera Sugar itakuwa ngumu, wamejipanga kucheza kwa kumuheshimu mpinzani na muhimu kwao ni alama 3

"Kwa upande wetu sisi tumejiandaa vizuri na kila mchezaji anafahamu umuhimu wa Mchezo wa Kesho. Kikubwa ni kwamba tunawaheshimu sana Kagera Sugar kwasababu wana timu nzuri inayoleta Ushindani kwenye Ligi"

"Watakuja kuonesha ubora wao hivyo tunaamini utakuwa mchezo mzuri, Wananchi wategemee mazuri kutoka kwetu," alisema

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’