Local,Normal News,KenGold, Yanga

Morrison kuikosa Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Feb 2025
Morrison kuikosa Yanga

Nyota mpya wa KenGold, Bernard Morrison ‘BM3’, huenda akakosa baadhi ya michezo ya kikosi hicho baada ya kupewa programu maalumu za mazoezi na kocha mpya wa timu hiyo, Mserbia Vladislav Heric, kabla ya kuungana na mastaa wenzake kikosini.

Daktari wa KenGold, Amina Iddy Turusa amesema nyota huyo kapewa program maalumu za mazoezi, huku akishindwa kuweka wazi kama ni majeruhi na anaweza akakosa michezo ijayo ya kikosi hicho hususani ujao wa Yanga.

Kwa upande wa Ofisa Habari na Mawasiliano wa KenGold, Joseph Mkoko alisema wachezaji wote wako fiti kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Yanga, huku akikiri ni kweli nyota huyo amepewa programu na benchi la ufundi na anaendelea pia vizuri.

"Mambo mengine ni ya ndani na nisingependa kuyaweka wazi, itoshe kusema ni kweli anaendelea na mazoezi binafsi na suala la yeye kucheza au kutocheza dhidi ya Yanga, hilo litabakia maamuzi ya benchi la ufundi ila nyota wetu wote wako fiti," alisema

Morrison ni miongoni mwa nyota waliobeba matumaini ya kikosi hicho baada ya kusajiliwa dirisha dogo akiungana na mastaa wengine waliotamba na Yanga na Simba wakiwemo beki, Kelvin Yondani, kiungo, Zawadi Mauya na mshambuliaji, Obrey Chirwa.

KenGold inayoburuza mkiani na pointi sita tu katika michezo 16 iliyocheza, itacheza dhidi ya Yanga Jumatano ya Februari 5, kwenye Uwanja wa KMC Complex, huku ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mechi ya kwanza bao 1-0, Septemba 25, mwaka jana.

Nyota huyo wa zamani wa Simba na Yanga aliyewahi pia kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini, DR Congo na Morocco ni kati ya mwa wachezaji 24 waliosajiliwa na kutambulishwa hivi karibuni waliobeba matumaini ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu kwa msimu wa kwanza ikitoka Ligi ya Championship.

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’