International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu February 10 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Feb 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu February 10 2025

Arsenal na Tottenham wote wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Fiorentina na Italia Moise Kean mwenye umri wa miaka 24. (Nicolo Schira)

Manchester United na Aston Villa zote zilikuwa tayari kutoa euro 70m (Β£58.3m) kwa Fermin Lopez wa Barcelona mwezi Januari, lakini mshambuliaji huyo wa miaka 21 wa Uhispania hakutaka kuhama. (Sport – In Spanish)

Barcelona ilikataa ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ureno Joao Felix katika dirisha la uhamisho la Januari kabla ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kusaini mkataba wa mkopo kwenda AC Milan hadi mwisho wa msimu. (Sport – In Spanish)

Arsenal wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ureno Diogo Jota, huku Liverpool wakiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa ada sahihi kwa sababu ya idadi ya michezo ambayo amekosa kutokana na jeraha. (Anfield Watch)

Atletico Madrid wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 27, ambaye mkataba wake na The Eagles utakamilika 2026. (Teamtalk)

Hata hivyo, Mmiliki wa Lyon Mmarekani John Textor, ambaye ni mwanahisa mkuu katika Crystal Palace, anataka timu yake ya Ligue 1 kuwasilisha zabuni kwa Mateta yenye thamani ya pauni milioni 50. (Sun)

Crystal Palace wamemlenga beki wa Burnley Mfaransa Maxime Esteve, 22, na mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi wa Middlesbrough Rav van den Berg, 20, kama mbadala wa beki wa kati wa England, 24, Marc Guehi (Sun)

Everton inalenga kuwasajili nyota chipukizi wa Uingereza kama sehemu ya mpango mpya wa usajili. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
3m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
32m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’