International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Februari 19 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Feb 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Februari 19 2025

Manchester United wanamtaka mshambuliaji wa timu ya vijana ya England chini ya miaka 21 kutoka Ipswich Town, mwenye thamani ya Pauni milioni Β£40m, Liam Delap mwenye miaka 22

Delap, ambaye alitoka timu ya vijana ya Manchester City, ambaye amefunga mabao 10 katika ligi kuu ya England msimu huu na pia anaswakwa na Chelsea pia. (i Paper)

Liverpool iko tayari kumtoa mshambuliaji wake Mruguay, Darwin Nunez, 25, pamoja na fedha, ili kumnasa mshambuliaji Msweden, Alexander Isak, 25, kutoka Newcastle, ambaye ana thamani ya pauni milioni Β£40m100m. Isak amefunga mabao 17 kwenye ligi kuu England msimu huu. (Football Insider)

Hata hivyo, Newcastle haitaruhusu wachezaji wake huyo bora kuondoka iwapo hawafanikiwi kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. (Daily Mail)

Arsenal na Chelsea wanavutiwa na mshambuliaji wa Ufaransa anayekipiga Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, 22, kama mbadala wa Isak. (CaughtOffside)

Liverpool inamuania pia kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi, Frenkie de Jong, 27, ikimuweka kwenye orodha ya wachezaji ambao Reds inawataka kuwasajili kwenye dirisha lijalo la majira ya joto. (Teamtalk)

Meneja wa Bournemouth, Andoni Iraola, ambaye amewafanya mashabiki wa timu hiyo kuwa na ndoto za kushiriki michuano ya Ulaya, yupo kwenye orodha ya makocha wanaosakwa na Tottenham iwapo wataamua kumtimua Ange Postecoglou, ambaye amekuwa akiinoa timu hiyo tangu Juni 2023, lakini yupo kwenye kuti kavu kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo. (Talksport)

Kiungo kutoka Argentina wa Manchester City, Maximo Perrone, 22, anayecheze Como kwa mkopo anataka kuhamia moja kwa moja kwenye timu hiyo ya Italia - inayoongozwa na mchezaji wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Cesc Fabregas. (Calcioline - in Italian)

Kiungo wa kati ya wa AC Milani, Mholanzi Tijjani Reijnders, 26, atasaini mkataba mpya kusalia katika klabu hiyo ya Italia hadi mwaka 2030. (Fabrizio Romano on X)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’