Local,Normal News,Namungo, Simba

Fadlu apania alama tatu Ruangwa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Feb 2025
Fadlu apania alama tatu Ruangwa

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa leo Jumatano, Februari 19 katika uwanja wa Majaliwa huko Ruangwa

Akizungumza jana katika Mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Fadlu amesema wanakwenda kukabiliana na timu ngumu ambayo ni imara katika safu ya ulinzi hivyo mpango wa mechi hiyo ni kutengeneza mashambulizi mengi na kutumia kila nafasi

Fadlu ameeleza kuridhishwa na kiwango cha kikosi chake katika mechi zilizopita akiwa na imani wataendeleza ubora wao katika mchezo huo

"Tumekuwa na muda wa kutosha kujiandaa na mchezo dhidi ya Namungo Fc, tuko tayari kwa mchezo huu"

"Nafurahi tumeendelea kuimarika na kuwa bora kutoka mechi moja hadi nyingine"

"Kesho (leo) tunakwenda kukabiliana na mpinzani mgumu mwenye safu nzuri ya ulinzi hivyo tutapaswa kuwa kwenye ubora wetu katika ushambuliaji"

"Malengo yetu ni kuona tunashinda mchezo huu ambao nafahamu hautakuwa mwepesi," alisema Fadlu

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake mlinzi wa kulia David Kameta 'Duchu' amesema morali ya wachezaji iko juu na malengo yao ni kuibuka na ushindi mnono

"Morali ya wachezaji wote iko juu kuelekea mchezo huo. Tunafahamu msimu uliopita hatukupata ushindi katika uwanja wa Majaliwa, tunalijua hilo hivyo tumejiandaa kufanya vizuri"

"Sasa tuna walimu tofauti na msimu uliopita, kitu kikubwa tunakwenda kupambana malengo yetu ni kupata alama tatu katika kila mchezo," alisema

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’