Yanga yaifuata Mashujaa Fc, Kigoma

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st February 2025


Yanga yaifuata Mashujaa Fc, Kigoma

Kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es salaam mapema leo Ijumaa kuelekea mkoani Kigoma tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc ambao utapigwa Jumapili, Februari 23 katika uwanja wa Lake Tanganyika

Msafara wa Yanga umejumuisha wachezaji 21, benchi la ufundi na baadhi ya viongozi waandamizi wa klabu hiyo

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wanakwenda Kigoma wakiwa na lengo moja, kushinda mchezo dhidi ya Mashujaa Fc na kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi

Yanga ndio vinara wa ligi kuu ya NBC wakikusanya alama 52 baada ya mechi 20


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.