International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu, Februari 24 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Feb 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu, Februari 24 2025

Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, amewataka viongozi wa klabu hiyo kumsajili winga wa timu ya vijana ya Ureno chini ya miaka 21, Geovany Quenda, mwenye umri wa miaka 17, kutoka klabu yake ya zamani Sporting kwa dau la pauni milioni 35 (Star)

West Ham wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Southampton, Taylor Harwood-Bellis, mwenye umri wa miaka 23 na anayewakilisha timu ya taifa ya England (Sun - subscription required)

Real Madrid bado wanamtaka Jarrad Branthwaite lakini wanasita kutoa dau la pauni milioni 62 wanalotaka Everton kwa ajili ya kumuuza beki huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 22. (Diario AS - in Spanish)

Crystal Palace wanavutiwa na usajili wa mshambuliaji wa Liverpool, Lewis Koumas, mwenye umri wa miaka 19 na anayeichezea Wales, pamoja na winga wa Scotland mwenye umri wa miaka 19, Ben Doak, ambao kwa sasa wako kwa mkopo katika timu za Stoke na Middlesbrough, mtawalia. (Alan Nixon)

Real Madrid wanataka kumbakiza Luka Modric na wako tayari kumpa kiungo huyo wa Croatia, ambaye atatimiza miaka 40 mwezi Septemba, mkataba mpya. (Nicolo Schira)

Tottenham wako tayari kumuuza Manor Solomon msimu huu wa kiangazi, huku Leeds, ambako winga huyo wa Israel mwenye umri wa miaka 25 yuko kwa mkopo pamoja na Everton wakionesha nia ya kutaka kumsajili. (Givemesport)

Liverpool wanatumai kuwashinda Arsenal katika umsajili wa kiungo kinda wa Rosenborg, Sverre Nypan, mwenye umri wa miaka 18 na anayechezea timu ya taifa ya Norway chini ya miaka 21. (Fichajes - in Spanish)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
35m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’