International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi March 1 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Mar 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi March 1 2025

Arsenal wanataka kumsajili kiungo wa Bayern Munich na Ujerumani, Joshua Kimmich, 30, kwa uhamisho huru majira ya kiangazi. (Sky Sports)

The Gunners wameonyesha nia thabiti ya kumsajili Kimmich, huku makubaliano ya kumsajili kiungo wa Hispania, Martin Zubimendi, 26, kutoka Real Sociedad yakielekea kukamilika. (Metro). Liverpool na Barcelona pia zinavutiwa na Kimmich. (Sun)

Aston Villa wamejiunga na Arsenal katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Serbia, Dusan Vlahovic, 25, ambaye anaonekana kuwa karibu kuondoka Juventus majira ya kiangazi. (TeamTalk)

Liverpool wanapanga kumsajili beki wa kati na beki wa kulia katika dirisha la majira ya kiangazi, bila kujali mustakabali wa beki wa Uholanzi, Virgil van Dijk, 33, huku beki wa kimataifa wa England, Trent Alexander-Arnold, 26, akitarajiwa kuhamia Real Madrid. (Football Insider)

Liverpool wanaweza kumruhusu winga wa Colombia, Luis Diaz, kuondoka kwa dau la takriban euro milioni 70 (Β£57.7m) majira ya kiangazi, huku Atletico Madrid wakionesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Fichajes - in Spanish)

Chelsea hawana mpango wa kusajili kipa katika dirisha la majira ya kiangazi, licha ya ukosoaji wa hivi karibuni dhidi ya kipa wa Hispania, Robert Sanchez, 27, na kipa wa Denmark, Filip Jorgensen, 22. (Times - subscription required)

Arsenal wanaweza kuelekeza macho kwa mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, 21, kama chaguo la gharama nafuu zaidi badala ya mshambuliaji wa Newcastle United, Alexander Isak, hali ambayo inaweza kumpa Liverpool fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Sweden, Isak, 25, kutoka kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu. (Liverpool Echo)

Kiungo wa Manchester United na Brazil, Casemiro, 33, ni mmoja wa wachezaji wanaolengwa na AC Milan katika usajili wa majira ya kiangazi. (Fichajes - in Spanish)

Newcastle hawana mpango wa kupokea ofa kwa beki wa kulia wa England, Tino Livramento, 22, licha ya kuwaniwa na Manchester City. (Football Insider)

Arsenal wanaweza kushindana na AC Milan katika kumsajili beki wa kushoto wa Wolves na Algeria, Rayan Ait-Nouri, 23. (CaughtOffside)

Everton hawatarajiwi kumsajili winga wa Leeds United, Jack Harrison, 28, kwa mkataba wa kudumu baada ya kumaliza muda wake wa mkopo. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
35m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’