Local,Normal News,Yanga

Kocha Yanga hataki wakaa benchi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Mar 2025
Kocha Yanga hataki wakaa benchi

Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi, amesema hadi kufikia Mei mwaka huu, hakuna mchezaji yeyote wa Yanga aliyesajiliwa msimu huu ambaye hatapata nafasi ya kucheza kwenye mchezo wowote wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Kocha huyo amesema anataka wachezaji wote waliosajiliwa wacheze na waipe mafanikio klabu, kuwafurahisha mashabiki na wao wenyewe kutengeneza wasifu wao kwa maisha yao ya baadaye kwenye soka

Miloud aliyasema hayo jijini Dar es Salaam juzi, huku akifafanua kwamba amekuwa akifanya mabadiliko ya wachezaji wengi kipindi cha pili kwenye kikosi cha Yanga tangu aanze kukinoa kwani anahitaji awaone wachezaji wote, viwango vyao, ili aweze kuchukua maamuzi sahihi mwishoni mwa msimu

Alisema anawaheshimu wachezaji wote aliowakuta, hivyo atawapa nafasi wamwoneshe walichonacho, huku akisema hapendi wachezaji ambao wanaridhika na kukaa benchi

"Nataka hadi kufika Mei, wachezaji wote waliosajiliwa Yanga wawe wamecheza mechi za Ligi Kuu na Kombe la FA. Nimeanza kuwatengeneza wachezaji wote wawe wana uwezo wa kuisaidia timu kwani hawakusajiliwa Yanga kwa ajili ya mafunzo, bali kuja kufanya kazi, kuisaidia klabu kwenye malengo yake, kuwafurahisha mashabiki na wao wenyewe wasonge mbele kwenye maisha yao ya soka," alisema kocha huyo

Miloud, alipewa mikoba ya kuifundisha Yanga baada ya kuondoka kwa Sead Ramovic, ambaye ametimkia CR Belouizdad ya Algeria

Kabla ya kutua Yanga, alikuwa kocha wa Singida Black Stars, ambako hakuwahi kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo wowote wa Ligi Kuu

Kocha huyo ameiongoza Yanga kwenye michezo mitano ya Ligi Kuu, akishinda minne na kutoka sare mmoja. Alianza na mguu mbaya, timu yake ikitoka suluhu dhidi ya JKT Tanzania, Februari 10, mwaka huu, lakini baada ya hapo, alipata ushindi wa michezo minne mfululizo, akiiongoza Yanga kushinda mabao 6-1 dhidi ya KMC, 2-1 dhidi ya Singida Black Stars, 5-0 dhidi ya Mashujaa FC na 3-0 dhidi ya Pamba Jiji

Akiwa Kocha Mkuu, ameiwezesha Yanga kuvuna pointi 13, mabao 16, ikiruhusu nyavuni kwake mabao matatu pekee

IPP Media

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
35m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’