International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne March 04 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Mar 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne March 04 2025

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anatarajiwa kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wa Uingereza Jack Grealish, 29, huku kukiwa na mipango ya kukimarisha kikosi cha City. (Football Insider)

Inter Milan wanaibuka wapinzani wakuu wa klabu ya Liverpool katika mbio za kumsajili kiungo wa Ujerumani Joshua Kimmich huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akiingia akisalia na miezi michache katika mkataba wake na Bayern Munich. (Team Talk)

Chelsea inamfuatilia kwa karibu kipa wa Uholanzi na klabu ya Brighton Bart Verbruggen, 22, kwa ajili ya uhamisho wa majira ya joto. (GiveMeSport)

Manchester United, Tottenham na Arsenal zimeonyesha nia ya kumsajili Benjamin Sesko kutoka RB Leipzig, na mshambuliaji huyo wa Slovenia mwenye umri wa miaka 21 ana kipengele cha kutolewa ambacho kinaweza kutumika msimu huu wa joto. (Sky Sport Germany)

Mshambuliaji wa Brighton wa Brazil Joao Pedro, 23, anataka kujiunga na Liverpool majira ya joto. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Canada Jonathan Davidyuko tayari kuondoka katika klabu hiyo kama mchezaji huru msimu huu wa joto. (Nicolo Schira)

Wasaka vipaji wa Real Madrid wamekuwa wakimfuatilia kiungo wa England Adam Wharton tangu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 arejee kwenye kikosi cha kwanza cha klabu ya Crystal Palace. (Mail)

Liverpool wameanza mazungumzo na Conor Bradley kuhusu kandarasi mpya ya miaka mitano ambayo itamuwezesha beki huyo wa Ireland Kaskazini, 21, kupata nyongeza ya 650%. (Sun)

Brentford na Fulham zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa Mexico Johan Vasquez, 26, kutoka Genoa. (GiveMeSport)

Fulham na Sporting wanamuwinda beki wa Ugiriki, Georgios Vagiannidis, huku Sporting wakiwasilisha dau la euro 10m (Β£8.3m) kwa Panathinaikos. (Football Insider)

Beki wa Ujerumani Jonathan Tah, 29, ataondoka Bayer Leverkusen kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu. (Nicolo Schira)

Gwiji wa zamani wa a Atletico Madrid Andrea Berta anaaminika kuwa miongoni mwa watu wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya Edu kama mkurugenzi wa michezo wa Arsenal. (Telegraph - usajili unahitajika)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’