Local,Normal News,Yanga, Simba

Yanga yakomaa CAS, Bodi ya ligi yanena

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Mar 2025
Yanga yakomaa CAS, Bodi ya ligi yanena

Sakata la kuahirishwa kwa mechi ya Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba, iliyokuwa ichezwe Machi 8, 2025, limechukua sura mpya

Awali, suala hili lilionekana kama masihara, lakini sasa linaonekana kuingia katika hatua nzito

Yanga imewasilisha rasmi kesi hiyo katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) jijini Lausanne, Uswisi, baada ya kutoridhishwa na majibu ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)

Licha ya hatua hiyo, hakuna kiongozi yeyote aliyekubali kunukuliwa kwa jina, wakidai kuhofia mamlaka za soka na serikali

Hata hivyo, inadaiwa kuwa CAS itawasiliana rasmi na TFF pamoja na Bodi ya Ligi ili kuthibitisha kupokea rufaa hiyo

Yanga inasisitiza kuwa haijaridhika na maamuzi ya ndani, hivyo imechukua hatua hiyo kutafuta haki kwenye chombo cha juu zaidi cha usuluhishi wa michezo duniani

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto, amesema tayari wamejibu barua ya Yanga na hawana mamlaka ya kuwazuia kwenda CAS lakini kama wameenda CAS kwa kipindi hiki ambapo hawajasema kuwa hilo suala limeamriwa vipi itakuwa ni kitu cha kuchekesha, akisisitiza kuwa maamuzi ya mwisho ya bodi bado hayajatolewa

Mnguto amesema anaamini suluhu inaweza kupatikana kupitia vikao vya ndani. Ameeleza kuwa busara na hekima zinapaswa kutumika ili kila upande uridhike badala ya kupeleka suala hilo nje ya nchi

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
3m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
32m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’