Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' usiku wa leo kuelekea kesho majira ya saa 6:30, itakuwa uwanjani huko Morocco kupepetana na wenyeji wao Morocco katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la Dunia 2026
Hii ni mechi muhimu kwa Tanzania kuhakikisha haipotezi ili kuwa na matumaini ya kuwania nafasi hiyo katika kundi E
Morocco ndio vinara wa kundi hilo wakikusanya alama 12 baada ya kushinda mechi zote nne wakati Tanzania ikishika nafasi ya tatu ikiwa na alama 6 sawa na Niger ambayo imefunga mabao mengi zaidi
Hata hivyo Niger wamecheza mechi nne wakati Stars ikicheza mechi tatu, leo itakamilisha mechi ya nne
Kama Stars hawatapoteza mchezo leo watakuwa na uhakika wa kusogea hadi nafasi ya pili
Hata hivyo haitakuwa kazi rahisi mbele ya Taifa bora zaidi kwenye soka Afrika kwa sasa
Ikiwa chini ya makocha wazawa Hemed Morocco, Juma Mgunda na Jamhuri Kiwhelo 'Julio', Stars imepania kuwaduwaza Morocco katika ardhi yao