Local,Normal News,Simba

Mo awaita mashabiki Simba kwa Mkapa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 Apr 2025
Mo awaita mashabiki Simba kwa Mkapa

Rais wa heshima wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amesema wakati huu Simba inahitaji umoja na ushiriano kutoka kwa kila Mwanasimba ili kuhakikisha wanashinda mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry

Jumatano, April 09, Simba itakuwa mwenyeji wa Al Masry katika ambao Simba inahitaji kushinda angalau mabao matatu ili kufuzu nusu fainali

Mo amesema hii ni mechi muhimu na kihistoria kwa Simba hivyo ni muhimu mashabiki kujitokeza kwa wingi kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa

"Hii Tunavuka. Kwa neema na mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Huu ni mchezo wa kihistoria. Na kila mmoja wetu ana nafasi ya kuwa sehemu ya ukurasa huu wa Simba"

"Tunachohitaji sasa ni UMOJA. Mashabiki wote wa Simba, tunawaomba mjitokeze kwa nguvu zote. Tujaze uwanja. Ili mioyo ya wachezaji wetu ipate nguvu na ujasiri wa kupigana hadi mwisho"

"Kwa pamoja tutapambana na Inshallah, Tutavuka," aliandika Mo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Baada ya kucheza robo fainali ya michuano ya CAF kwa misimu mitano mfululizo, wakati huu Wanasimba wanasema imetosha na wanaitaka nusu fainali

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
8h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
12h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
15h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
16h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
17h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
19h ago
READ MORE β†’