International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi April 10 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
10 Apr 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi April 10 2025

Manchester City wanatazamia kufufua shauku yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle na Brazil Bruno Guimaraes, 27, wakati wanajiandaa kuondoka kwa Mbelgiji Kevin de Bruyne, 33. (UOL esporte)

Chelsea wako tayari kulipa euro 120m (Β£102m) ili kumsajili winga wa Real Madrid na Brazil Rodrygo, 24, kama mchezaji wao nyota msimu wa joto. (Fichajes)

Manchester City wanafikiria kutoa kati ya euro 50-60m (Β£42-51m) kwa kiungo wa AC Milan na Uholanzi Tijjani Reijnders, 26, licha ya hivi karibuni kusaini mkataba mpya hadi 2030. (Calciomercato)

Everton wanatarajia kumpoteza mlinzi wa kati wa England Jarrad Branthwaite, 22, msimu huu huku Manchester United na Tottenham zikimtaka. (Sun)

Chelsea na Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Benfica na Ugiriki Vangelis Pavlidis, 26, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Barcelona na Atletico Madrid. (Record)

Arsenal na Liverpool wanatafuta mbadala wa Alexander Isak huku Newcastle wakisisitiza kwamba hawatamuuza mshambuliaji wao wa Sweden mwenye umri wa miaka 25. (i paper)

Newcastle, Wolves na Brentford wanamtazama mlinda lango wa Angers na Ivory Coast Yahia Fofana, 24, kabla ya uhamisho wa pauni milioni 15 msimu wa joto. (Football Insider)

Chelsea wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Sunderland na England chini ya umri wa miaka 21 Jobe Bellingham, 19, mbele ya Manchester United, Arsenal, Tottenham, Brighton na Crystal Palace. (Caught Offside)

Leeds itasikiliza ofa kwa ajili ya mlinda lango wa Ufaransa Illan Meslier, 25, na kutumia fedha hizo kusajili mbadala wa chaguo la kwanza. (Football Insider)

Juventus wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, msimu wa joto, lakini wanataka karibu euro 40m (Β£34m). (Tuttosport)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’