International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa April 11 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Apr 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa April 11 2025

Manchester City wamemuongeza mlinzi wa kushoto wa Tottenham na Italia Destiny Udogie, 22, kwenye orodha fupi ya wachezaji wanaotarajiwa kusajiliwa huku wakipania kuimarisha nafasi ya mlinzi wa pembeni msimu huu. (Fabrizio Romano)

Meneja wa Lens Mwingereza aliyezaliwa Ubelgiji, Will Still, 32, ni miongoni mwa wanaowania kuwa meneja mpya wa Southampton kufuatia kuondoka kwa Ivan Juric mapema wiki hii. (Talk sport)

Arsenal, Chelsea, Liverpool, Newcastle na Spurs wamekutana au kufanya mazungumzo na wawakilishi wa mlinzi wa Uhispania mzaliwa wa Uholanzi Dean Huijsen, kabla ya uamuzi kufanywa kuhusu hatma ya mchezaji huyo wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 19. (Athletic)

West Ham wanafikiria kumnunua mlinda lango wa Southampton na Uingereza Aaron Ramsdale, 26 msimu wa joto. (Times )

Real Betis wanashikilia pauni milioni 35 huku Chelsea wakiongeza nia ya kumnunua winga wa Uhispania Jesus Rodriguez, 19. (Mail, external)

Newcastle wanatayarisha ofa kwa mlinda lango wa Burnley James Trafford, 22, na wanataka kumsajili Muingereza mwenzake Dominic Calvert-Lewin, 28, huku mkataba wa mshambuliaji huyo katika Everton ukimalizika mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider )

Klabu ya Uholanzi ya PSV Eindhoven ina nia ya kutaka kumnunua winga wa Ipswich Muingereza Jack Clarke, 24, msimu huu wa joto. (Football Insider)

Atalanta itatarajia kuanza ofa ya zaidi ya Β£51m (euro milioni 60) kwa mshambuliaji wa zamani wa Everton Ademola Lookman, 27, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Italia mwishoni mwa msimu huu. (Calciomercato)

Barcelona wamepunguza shauku yao ya kumnunua mlinzi wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah, 29, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Bundesliga unamalizika tarehe 30 Juni. (Sport )

Kocha wa Genoa Patrick Vieira yuko mbioni kuwa kocha mpya wa Roma, huku kiungo huyo wa zamani wa Arsenal na Ufaransa akiwa kwenye orodha ya wachezaji wanne wanaowania kibarua hicho. (Sky Sport Italia )

Mkurugenzi wa soka wa Barcelona Deco amemteua mchezaji wa kimataifa wa Uhispania wa Real Sociedad Alex Remiro, 30, kuchukua nafasi ya Mjerumani Marc-Andre ter Stegen, 32, kwa nafasi ya mlinda lango wa klabu hiyo. (Catalunya Radio)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’