Local,Normal News,Simba

Simba yatangaza viingilio mchezo dhidi ya Stellenbosch

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Apr 2025
Simba yatangaza viingilio mchezo dhidi ya Stellenbosch

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali metangaza viingilio vya mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) dhidi ya Stellenbosch utakaopigwa Jumapili, April 20 katika uwanja wa New Amaan Complex

Ahmed ametangaza viingilio hivyo mapema leo visiwani Zanzibar katika Mkutano na waandishi wa habari

"Uwanja wa Amaan unaingiza watu 15,885. Viingilio ni VIP A - Tsh. 40,000, VIP B - Tsh. 20,000 na Mzunguko ni Tsh. 10,000. Tiketi zitauzwa kwa mfumo wa N-Card. Kuanzia hivi sasa tiketi zinapatikana katika maeneo mbalimbali. Kwa wale wa Dar es Salaam vituo vyote ambavyo vinauza tiketi vitaendelea kuuza tiketi kama kawaida"

"Kwa ndugu zangu wa Zanzibar ambao wamezoea kununua tiketi za karatasi kwasasa wanaweza kununua tiketi za N-Card na ukawa nayo hadi siku ya mchezo. Siku ya mchezo tiketi hazitauzwa nje ya uwanja na maeneo mengine yataendelea. Utaratibu huu ni wa CAF. Yeyote ambaye anahitaji tiketi anunue tiketi sasa"

"Hii Simba inayokuja kucheza Zanzibar ni mpya kabisa, Watu wa Dar wao wameshaiona kwenye mchezo wa robo fainali. Sizungumzii kuangalia kwenye TV, kuangalia live. Simba ya nusu fainali ni nyingine kabisa, mnaenda kushuhudia kila kitu kipya. Hii sio mechi ya mtu kuangalia kwenye tv, sio mechi ya kuhadithiwa, hii ni mechi ya kuangalia kwa macho ya nyama. Hii ni mara ya kwanza Simba ikiwa katika nafasi ya nne kwa ubora Afrika kucheza"

"Muda mzuri wa mazishi huwa ni saa 10 jioni, muda mzuri wa kumzika mtu huwa ni saa 10 na sisi muda wetu tukitaka kufanya Ubaya Ubwela na huwa tunafanikiwa kabisa huwa ni saa 10 jioni. Tukutane Uwanja wa Amaan, mechi ni sa 10:00 jioni. Wanaotoka Dar es Salaam wajue kabisa muda wa mchezo wasijesema wamekariri muda wa saa 2:15 usiku," alisema Ahmed

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
30m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’