Leo hii katika uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban, mechi ya kukata na shoka itapigwa wakati Stellenbosch FC wakimenyana na Simba SC katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.
Simba wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki iliyopita kwenye Uwanja wa New Amaan huko Zanzibar.



