Local,Normal News,Mtibwa

Mtibwa Sugar wamerudi ligi kuu, watadumu?

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Apr 2025
Mtibwa Sugar wamerudi ligi kuu, watadumu?

Mtibwa Sugar imehitaji msimu mmoja tu kurejea katika ligi kuu ya NBC baada ya juzi kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Bigman FC kwenye Uwanja wa Ilulu Lindi

Wakata miwa hao kutoka mkoani Morogoro wamekuwa timu ya kwanza kukata tiketi hiyo huku ikisaliwa na michezo miwili mkononi kuhitimisha msimu wa 2024-2025.

Mtibwa iliyoshuka daraja msimu uliopita sambamba na Geita Gold, imepanda kufuatia Stand United kulazimishwa suluhu ugenini na Cosmopolitan.

Mtibwa Sugar imefikisha pointi 67 baada ya kucheza michezo 28, hivyo timu pekee inayoweza kuzifikia ni Mbeya City iliyoichapa Geita Gold mabao 3-2, ambapo ikishinda mechi zake zote mbili zilizobakia itafikisha pointi 68.

Kwa maana hiyo, suluhu ya Stand United inaiweka nafasi ya tatu na pointi 59 ambapo hata ikishinda michezo yake miwili iliyobakia itaishia na 65, hivyo itakuwa na kinyang'anyiro cha kuwania michezo ya 'Play-Off' kusaka tiketi ya kupanda tu

Wakati Mtibwa Sugar ikijihakikishia kurejea ligi kuu, KenGold iliyopanda daraja msimu uliopita nayo tayari imejihakikishia tiketi ya kucheza Championship msimu ujao

Β 

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’