International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne April 29 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Apr 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne April 29 2025

Arsenal wanafikira kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Christopher Nkunku, 27, ambaye hayuko katika mipango ya timu ya Chelsea kwa sasa, huku Mikel Arteta akitafuta kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji msimu huu wa kiangazi. (Teamtalk)

DC United wamekuwa kwenye mazungumzo ya mkataba kwa miezi kadhaa na kiungo wa zamani wa Manchester United, Juventus na Ufaransa Paul Pogba, 32, ambaye hajacheza soka kwa miezi 20. (Washington Post)

Mabingwa wa Ligi Kuu England Liverpool wanatarajia kuwekeza kiasi kikubwa kwenye kikosi chao msimu huu wa kiangazi, huku mshambuliaji wa kati na beki wa kushoto wakiwa kipaumbele chao cha kwanza. (Telegraph)

Chelsea wanapanga kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jamie Gittens, 20, raia wa Uingereza, kabla ya Kombe la Dunia la Klabu, na kuna uwezekano wakamuuza mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 25, kwa klabu hiyo ya Ujerumani kama sehemu ya mpango huo.

Sancho kwa sasa yuko kwa mkopo Stamford Bridge kutoka Manchester United, lakini Chelsea wana wajibu wa kufanya mkataba huo kuwa wa kudumu. (Teamtalk)

Rais wa Real Sociedad Jokin Aperribay amesema mustakabali wa kiungo wa kati wa Hispania Martin Zubimendi, 26, ambaye anasakwa na Arsenal, utaamuliwa mwezi Juni. The Gunners wako tayari kuanzisha mchakato wa kulipa pauni milioni 51. (Radio Marca Donostia)

Everton wamemweka mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na Brazil Richarlison, 27, kama kipaumbele chao kikuu msimu huu wa kiangazi. (Givemesport)

Kiungo wa Newcastle raia wa Uingereza Sean Longstaff, 27, anasakwa na Leeds United. (i Paper)

Spurs italazimika kuuza wachezaji ili kupata fedha kwa ajili ya usajili mpya msimu huu wa kiangazi. (Telegraph) Mwenyekiti wa Leeds Paraag Marathe anasafiri kwenda Uingereza kufanya mazungumzo kuhusu mustakabali wa kocha Daniel Farke. (Guardian)

Fulham wanavutiwa kumsajili beki wa kulia wa England Kyle Walker-Peters, 28, kwa uhamisho wa bure pindi mkataba wake na Southampton utakapoisha msimu huu wa kiangazi. (Sky Sports)

Arsenal wako tayari kuanza mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Sporting na Sweden Viktor Gyokeres, 26, kuhusu uhamisho msimu huu wa kiangazi. (Givemesport)

Real Betis huenda ikashindwa kufikia bei ya Manchester United kwa ajili ya winga wa Brazil Antony licha ya klabu hiyo ya La Liga kuonyesha nia ya kufanya mkopo wake kuwa uhamisho wa kudumu. (Mirror)

Manchester United bado wanavutiwa kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 26, lakini kuna wasiwasi kuhusu mpango huo Old Trafford. (TBF Football)

Everton wako kwenye mazungumzo na kiungo wa Senegal Idrissa Gueye, 35, kuhusu mkataba mpya. (Football Insider)

Wrexham, Bolton, Charlton na Portsmouth wanavutiwa na mshambuliaji wa Dungannon Swifts kutoka Ireland ya Kaskazini Tomas Galvin, 20. (Football League World)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
35m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’