Mlinda lango Aboutwalib Mshery ameibuka shujaa kwenye mikwaju ya penati akiokoa mikwaju miwili muhimu na kuipeleka Yanga fainali ya kombe la Muungano baada ya ushindi wa penati 3-1 dhidi ya Zimamoto
Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 Yanga ikitangulia kufunga bao lake kwenye kipindi cha kwanza kupitia Maxi Nzengeli
Zimamoto walisawazisha katika kipindi cha pili kupitia mkwaju wa penati baada ya Mshery kumuangusha mshambuliaji wa timu hiyo katika eneo la hatari
Lakini unaweza kusema Mshery alisahihisha makosa yake na kuibeba Yanga mabegani katika mikwaju ya penati
Yanga sasa itachuana na JKU katika mchezo wa fainali utakaopigwa May 1