Local,Normal News,Yanga, Simba

Waziri Kabudi abanwa Bungeni sakata la Dabi ya Kariakoo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
7 May 2025
Waziri Kabudi abanwa Bungeni sakata la Dabi ya Kariakoo

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma ameishauri Serikali kuifanya Bodi ya ligi ijitegemee badala ya kuwachini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Mbali na ushauri huo, Msukuma pia amemtaka Waziri wa Michezo Profesa Paramagamba Kabudi kueleza alichokutana nacho ndani kwenye kikao cha maridhiano ya Simba na Yanga ambacho kilimfikisha saa nne za usiku

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 7,2025 wakati akichangia kwenye Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2025/26 ambapo Wizara imeomba Sh519.66 bilioni

Msukuma amewataka viongozi wa TFF kuiga mfano wa rais mstaa wa TFF Leodgar Tenga ambaye anasema alifanya kazi nzuri inayopaswa kuigwa hata kumfanya aendelee kuheshimika kwenye tasnia ya michezo nchini

'Alifanya kazi vizuri na ni mfano wa kuigwa, muige mfano jinsi alivyoongoza anaheshimika vinginevyo mtamaliza vipindi vyenu halafu mtakuwa mahohehahe hamjulikana mlichofanya,"amesema Msukuma

Amemtaka Waziri wa Michezo Profesa Kabudi kueleza kinagaubaga nini alichokutana nacho ndani ya kikao kilichowakutanisha viongozi wa Simba na Yanga ambacho kilimuweka hadi saa nne za usiku kwani imekuwa ni fumbo wakati watu wanataka kujua

"Ulichokisikia tueleza nasi tusikie ili tukawajulishe wananchi wetu, mpira wa Simba na Yanga ndiyo furaha, lakini kunapokuwa na migogoro halafu mnakuwa kimya na sijaona mahali popote ulipotaja migogoro hiyo hata mahali pamoja wakati Mheshimiwa Rais anajua mambo ya michezo na ametoa ndege kuwapeleka Simba Morocco," amesema.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’