Klabu ya Simba imetoa nafasi kwa mashabiki ambao wanataka kusafiri Morocco katika mchezo wa mkondo wa kwanza fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) dhidi ya RS Berkane ambao utapigwa May 17
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa ndege ambayo itaipeleka Simba Morocco na kuirejesha nchini baada ya mchezo
Simba imeanza kupokea maombi kwa wale ambao wangependa kusafiri na timu hiyo ili kuongeza hamasa kwenye mchezo huo wa mkondo wa kwanza



