Local,Normal News,Simba

Simba vs RS Berkane kupigwa kwa Mkapa au Amaan Complex?

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 May 2025
Simba vs RS Berkane kupigwa kwa Mkapa au Amaan Complex?

Ikiwa zimesalia siku chache kabla ya mchezo wa mkondo wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) dhidi ya RS Berkane ya Morocco, hali ya sintofahamu bado imetanda juu ya wapi mechi hiyo muhimu itapigwa.

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limepanga mchezo huo kufanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar, Jumapili, Mei 25, 2025 saa 12 jioni. Hata hivyo, Simba SC bado haijatoa tamko rasmi kukubali au kupinga uamuzi huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ali, ametoa ujumbe wa kutuliza mashabiki na wanachama wa klabu, akisisitiza kuwa juhudi kubwa zinaendelea kufanyika nyuma ya pazia ili kuhakikisha Simba inapata haki na mazingira bora ya kucheza mechi hiyo ya kihistoria katika uwanja wa Benjamin Mkapa

"Habari za Jumatatu Wana Simba wenzangu. Nafahamu wengi wetu tupo kwenye sintofahamu ya uwanja wa mechi yetu ya marudiano," aliandika Ahmed.

"Taarifa tuliyotoa awali ni kuwa klabu itatoa taarifa rasmi baada ya mchezo wetu wa kwanza kule Morocco. Viongozi wetu wa mamlaka zote wanapambana kuhakikisha jema kwa Simba linapatikana"

Ahmed alisisitiza kuwa uongozi wa klabu hauwezi kupokea tu maamuzi makubwa kama haya bila kufanya juhudi za kina kutafuta suluhu stahiki.

"Mabadiliko yenye athari kubwa kama haya huwezi kuyapokea tu bila kufanya juhudi. Hivyo basi niwaombe Wana Simba tuendelee kuwa watulivu. Ndani ya kipindi kifupi kijacho tutafahamu mustakabali wetu"

Pamoja na hali hiyo ya kutokuwepo kwa uhakika juu ya uwanja wa mchezo, Ahmed amewataka mashabiki waendelee kuipa nguvu timu yao kwa maandalizi ya kuwakabili Berkane kuendelea kama kawaida.

"Hata hivyo maandalizi ya kumtapisha Berkane yaendelee kama kawaida. Tunabebaaaaaaa – iwe chini ya bahari, iwe porini, iwe juu ya mlima – popote tunabebaaaaa," alimaliza Ahmed

Kwa sasa, macho na masikio ya mashabiki wa Simba SC na wapenda soka Tanzania yako kwa uongozi wa klabu hiyo ili kutoa tamko rasmi kuhusu uwanja utakaotumika, huku matumaini yakiwa kwamba watafanikiwa kurudisha mchezo huo uwanja wa Benjamin Mkapa

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
3h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
3h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
4h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
5h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
6h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
6h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
20h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
21h ago
READ MORE β†’