Local,Normal News,Simba, Berkane

Simba yaja na mikakati mipya ya kuikabili Berkane Zanzibar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 May 2025
Simba yaja na mikakati mipya ya kuikabili Berkane Zanzibar

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema baada ya jitihada za kurejesha mchezo wa mkondo wa pili fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) dhidi ya RS Berkane katika uwanja wa Benjamin Mkapa kukwama, hakuna tena muda wa kulalamika na sasa Simba inakwenda kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa Jumapili, May 25 katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya Simba, Osterbay jijini Dar es salaam, Ahmed alisema Simba ilipambana mchezo huo upigwe uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuwapunguzia gharama mashabiki wao ambao wengine wanasafiri kutoka mikoani

"Tuna mashabiki wamekata tiketi kutoka mikoa ya mbali, tathmni yetu ilionyesha pengine watahitaji kuwa na sio chini ya laki tatu kuweza kufika Zanzibar kushuhudia mchezo huo na kisha kurejea makwao"

"Lakini pia uwanja wa Benjamin Mkapa ungetoa nafasi ya mashabiki wengi zaidi kushuhudia mchezo huo wa kihistoria kwani watu 60,000 wangeingia uwanjani"

"Kwa kuwa jitihada zetu zimekwama, basi hatuna sababu ya kuendelea kulalamika. Lengo letu ya kutwaa ubingwa Afrika liko palepale kwa hiyo tunapaswa kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Berkane utakaopigwa Jumapili, May 25 katika uwanja wa New Amaan Complex, saa 10 jioni," alisema Ahmed

Ahmed amebainisha kuwa Kikosi cha Simba kitasafiri kesho Jumatano kwenda Zanzibar kwaajili ya kuanza maandalizi ya mchezo huo

Ahmed amesema kwa mashabiki ambao walikata tiketi kushuhudia mchezo huo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, watazitumia tiketi hizo katika Tamasha la Simba Day litakalofanyika baadae mwaka huu katika kuukaribisha msimu wa mashindano 2025/26

Utaratibu mpya wa viingilio umetangazwa ambapo viingilio vipya ni VIP 50,000/- URUSI 30,000/- na Mzunguuko 10,000/-

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’