Local,Normal News,Singida

Singida BS wafurahia kufuzu Shirikisho 2025/26

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 May 2025
Singida BS wafurahia kufuzu Shirikisho 2025/26

Kocha wa Singida Black Stars raia wa Kenya, David Ouma amesema kitendo cha kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao, kwao kama benchi la ufundi, viongozi na mashabiki ni jambo kubwa la kujivunia.

Timu hiyo imepata tiketi ya kushiriki michuano hiyo msimu ujao baada ya Yanga kuifunga JKT Tanzania mabao 2-0, katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), hivyo Singida Black Stars msimu huu kujihakikishia kumaliza ligi nafasi ya tatu au ya nne.

Kutokana na Tanzania kuwa na nafasi nne za uwakilishi wa michuano ya CAF, timu mbili za juu kwenye msimamo wa ligi huwa zinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na inayomaliza nafasi ya tatu inacheza Kombe la Shirikisho sambamba na bingwa wa Kombe la FA.

Kitendo cha Yanga na Simba kujihakikishia kumaliza nafasi ya kwanza na ya pili katika Ligi Kuu na hata zikichukua ubingwa wa Kombe la FA msimu huu, zitacheza Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam FC na Singida zilizopo ya tatu na nne zitacheza Kombe la Shirikisho.

Akizungumzia hilo, Ouma alisema moja ya malengo yao waliyojiwekea msimu huu ni kumaliza nafasi nne za juu na kushiriki michuano ya Afrika msimu ujao, hivyo kwa hapa walipofikia wanajivunia kwa sababu kile walichokikusudia wamekitimiza.

"Tunashukuru sana kwa hapa tulipofikia kwa sababu haya ndio malengo yetu tangu mwanzoni mwa msimu, tunaendelea kujipanga na mechi mbili ngumu zijazo dhidi ya Simba, hivyo niseme wazi maandalizi kijumla yako vizuri hadi sasa," alisema.

Ouma alisema wachezaji wote wamerejea kambini baada ya kutoa mapumziko ya siku nne na sasa wanajiandaa na mechi mbili mfululizo dhidi ya Simba za Ligi Kuu Bara itakayopigwa Mei 28, 2025 na ile ya nusu fainali ya Kombe la FA, Mei 31, 2025.

Ouma alianza kuiongoza timu hiyo Februari 4, 2025, baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Miloud Hamdi aliyetambulishwa Desemba 30, 2024, kuondoka kikosini na kutua Yanga anayoendelea kuifundisha.

Tangu Ouma akabidhiwe kikosi hicho kinachoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi na pointi 53, amekiongoza katika mechi 11 za Ligi Kuu Bara, kati ya hizo ameshinda sita, sare mbili na kupoteza tatu.

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
35m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’