Local,Transfer News,Yanga, Singida

Yanga yamkomalia Sowah

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 May 2025
Yanga yamkomalia Sowah

Klabu ya Yanga SC inaonekana kutopoteza muda katika maandalizi ya msimu ujao wa 2025/2026, baada ya kumuuza kiungo wao nyota Stephane Aziz KI, aliyejiunga na Wydad Casablanca ya Morocco, mabingwa hao wa Tanzania Bara wamepiga hatua kubwa kwa kuhakikisha wanaboresha safu ya ushambuliaji β€” na jina la Jonathan Sowah limewekwa kwenye mstari wa mbele.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, tayari mazungumzo ya siri baina ya viongozi wa Yanga na mshambuliaji huyo kutoka Ghana yamefanyika na kufikia makubaliano ya awali. Uwezekano ni mkubwa Sowah atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao, akiandaliwa mkataba wa miaka miwili

Sowah, ambaye kwa sasa anachezea Singida Black Stars, amekuwa moto wa kuotea mbali tangu alipojiunga na timu hiyo kupitia dirisha dogo la usajili mwezi Januari. Amecheza mechi 11 na kufunga mabao 11 β€” takwimu zinazothibitisha uwezo wake mkubwa wa kufumania nyavu.

Yanga, ambao wanaelekea kumuuza mshambuliaji chipukizi Clement Mzize kufuatia mvuto wake kwa vilabu vya Afrika na Ulaya, pia wanatarajia kuachana na Kennedy Musonda ambaye mkataba wake unatarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu huu. Hii itatoa nafasi ya usajili wa mchezaji wa kigeni kwa ajili ya kumpokea rasmi Sowah.

Inadaiwa kuwa, licha ya Sowah kuwa bado na mkataba na Singida Black Stars, mshambuliaji huyo mwenyewe kipaumbele chake ni kujiunga na Yanga kwani aliwahi kusema kwamba klabu ya Yanga ni 'nyumbani kwake'

Yanga inalenga kuunda safu ya mashambulizi itakayokuwa chini ya Jonathan Sowah na Prince Dube, wakitegemewa kuibeba timu hiyo katika harakati zake za kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’