Local,Normal News,Yanga, Simba

Serikali yaiachia TFF kumaliza sakata la dabi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Jun 2025
Serikali yaiachia TFF kumaliza sakata la dabi

Sakata la mchezo wa Dabi ya Kariakoo unaozikutanisha Yanga dhidi ya Simba, limeingia bungeni ambapo Serikali imesema haiwezi kuingilia kwa kuwa mchezo wa mpira wa miguu una kanuni zake kitaifa na kimataifa.

Kauli hiyo imekuja baada ya swali la nyongeza liloulizwa na Mbunge wa Makete (CCM), Festo Sanga aliloliuliza leo Juni 11,2025 wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni. Sanga amesema kuimarisha timu ya Taifa ni pamoja na kuhakikisha sheria na taratibu za michezo zinafuatwa.

β€œLigi yetu inaelekea mwisho lakini kumekuwa na mvutano wa hizi timu mbili (Yanga na Simba) na viongozi wa TFF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania), ipi kauli ya serikali?” Ameuliza Sanga.

Mh Mwinjuma alisema kama ambavyo wabunge wanafahamu shughuli za mchezo wa mpira wa miguu zina mamlaka zake za kitaifa na kimataifa.

β€œNa tumekuwa tukisisitiza mara kwa mara Serikali kutoingilia moja kwa moja uendeshaji wa shughuli hizo ili kuepuka kuja pengine hata kufungiwa na FIFA (Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa) katika nyakati hizi ambapo kitakwimu nchi yetu inafanya vizuri sana katika uendeshaji wa shughuli za mpira wa miguu,” amesema.

Amesema mamlaka za uendeshaji na usimamizi wa shughuli za mpira wa miguu nchini ziko chini ya TFF sambamba na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TLPB).

Amesema Serikali hata taarifa ambazo wanazitoa bungeni huwa wanapata taarifa kutoka katika mamlaka hizo kuhusu mchezo huo.

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
3m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
32m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’