Local,Normal News,Kengold

Afisa Habari KenGold anusurika kwenda jela

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Jun 2025
Afisa Habari KenGold anusurika kwenda jela

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya KenGold, Joseph Mkoko(34), kulipa faini ya Sh1 milioni au kwenda jela miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa.

Mkoko anadaiwa kuomba rushwa ya Sh1.5 milioni kutoka kwa mchezaji wa zamani wa timu ya mpira wa miguu ya Vital’O ya Burundi, ili amsaidie kusajiliwa na timu yake ya KenGold na kupata upendeleo wa kupangwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo amefanikiwa kulipa faini hiyo na hivyo kukwepa kifungo cha miaka miwili jela Hukumu hiyo imetolewa leo, Jumatano Juni 11, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Beda Nyaki, baada ya mshtakiwa huyo kukiri mashtaka yake.

Mshtakiwa huyo amekiri mashtaka yake wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili kusomewa hoja za awali, ambapo kabla ya kusomewa hoja za awali, alikumbushwa mashtaka yake kwa kusomewa upya na ndipo alipokiri mashtaka yake na mahakama hiyo kumtia hatiani.

Baada ya kutiwa hatiani, hakimu Nyaki alimhukumu. Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 13138 ya mwaka 2025 yenye mashtaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa.

Ofisa habari huyo anadaiwa kutenda makosa yake kati ya Disemba Mosi, 2024 hadi Disemba 31, 2024 eneo la Kibaha, mkoani Pwani.

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’