Mechi za mzunguuko wa 30 ligi kuu ya NBC zimetamatishwa leo miamba ya soka nchini Yanga, Simba na Azam Fc zikishinda mechi zao huku Prisons na Fountain Gate zikiangukia kucheza mechi za play-off
Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji ukiwa mchezo wa pili mfululizo Yanga ikishinda mabao matano baada ya kuichapa Prisons idadi hiyo ya mabao katika mchezo uliopita
Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni ikiwa na alama 79 sasa ikihitaji angalau alama moja tu kutwaa ubingwa
Watani zao Simba wameendelea kuweka hai matumaini yao katika mbio za ubingwa wakiichapa Kagera Sugar bao 1-0. Simba imefikisha alama 78, alama moja nyuma ya Yanga
Azam Fc imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Fountain Gate ikiendelea kusalia nafasi ya tatu
Huku Singida BS ikilazimishwa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Prisons na kusalia katika nafasi ya nne
Matokeo hayo hayakutosha kwa Prisons kuondoka eneo la play-off kama ilivyo kwa Fountan Gate

