Local,Normal News,Yanga, Simba

Bodi ya Ligi, Yanga wafunguka maandalizi ya dabi ya Kariakoo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Jun 2025
Bodi ya Ligi, Yanga wafunguka maandalizi ya dabi ya Kariakoo

Bodi ya ligi kwa kushirikiana na klabu ya Yanga na N-Card, wametangaza utaratibu wa mashabiki kuingia uwanjani katika mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Simba utakaopigwa Jumatano, Juni 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Karim Boimanda amesema umeandaliwa utaratibu mzuri kuhakikisha wale waliokata tiketi kwa ajili ya mechi ya mwanzo iliyopaswa kupigwa March 08 wanaingia uwanjaniΒ 

"Waliokata tiketi March 08 na tiketi hizo wanazo, wao watazitumia kuingia uwanjani siku ya Jumatano, Juni 25. Kwa wale ambao walikata tiketi lakini wamepoteza kadi, kuna utaratibu maalum umeandaliwa (swap) watapatiwa msaada geti A na geti B," alisema

Nae Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wanatambua umuhimu na ugumu wa mchezo dhidi ya Simba hivyo wanafanya maandalizi kikamilifu

"Yanga inafahamu ukubwa, ugumu na umuhimu wa mchezo dhidi ya Simba siku ya Jumatano. Hii ni kama zawadi kwa mashabiki kupata Kariakoo Derby yenye msisimko wa fainali"

"Sisi Yanga tuna faida mbili yaani tunahitaji ushindi au hata matokeo ya sare, huku wenzetu wakihitaji ushindi. Kwa wanachama na mashabiki wa Yanga hii ni mechi yetu kwa kuwa inakwenda kuamua hatma yetu msimu huu. Tunawakaribisha wanayanga waje kwa wingi"

"Tukiweza kuja kwa wingi tukaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa ni jambo kubwa zaidi. Tumefanya jitihada kubwa msimu huu kuisapoti timu yetu tangu mchezo wa kwanza. Na sasa wachezaji wetu wanatuhitaji tena katika mchezo muhimu ambao tunahitaji kupata matokeo mazuri ili tuweze kutwaa ubingwa," alisema Kamwe

Hata hivyo Kamwe hakuwa tayari kuweka wazi Yanga itarudi lini Dar es salaam huku akibainisha hata taarifa za kikosi hakupewa na viongozi lakini amewahakikishia Wanachama na mashabiki kuwa siku ya Jumatano Yanga itakuwa uwanjani kucheza dhidi ya Simba

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
33m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’