Local,Normal News,Yanga

Hamdi ahakikishiwa mkataba mpya Yanga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 Jul 2025
Hamdi ahakikishiwa mkataba mpya Yanga

Unaweza kusema kazi nzuri iliyofanywa na Kocha Miloud Hamdi imewapa sababu viongozi wa Yanga kumpa mkataba wa muda mrefu

Wakati Hamdi anatua Yanga kuchukua mikoba iliyoachwa na Sead Ramovic aliyetimkia CR Belouizdad, alisaini mkataba mfupi ambao umefikia tamati jana, Juni 30

Hata hivyo baada ya kuiongoza Yanga kutwaa kombe la CRDB juzi, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alimuhakikishia ameandaliwa mkataba mpya wa muda mrefu

Akizungumza jana Jangwani jijini Dar es salaam baada ya gwaride la ubingwa, Hamdi aliwashukuru mashabiki wa Yanga akikiri upendo wao kwa timu ni wa kipekee

"Nawashukuru sana mashabiki wa Yanga, mna upendo wa kweli kwa timu yenu, mnatuunga mkono kila hatua na kila sehemu tunayokwenda"

"Nimefanya kazi katika timu nyingi kubwa lakini niwaambie nyie ni watu wa kipekee. Leo tumekutana hapa kushangilia mafanikio yetu ya msimu huu"

"Lakini niwaambie kwa aina hii ya upendo mnaotuonyesha, tutapambana ili tukutane hapa kushangilia pamoja kila msimu," alisema Hamdi

Katika mechi 21 za mashindano ambazo Hamdi ameiongoza Yanga, ameshinda mechi 20 na kutoka sare mechi 1

Ameingoza Yanga kushinda mataji matatu yaani kombe la Muungano, Ligi Kuu na kombe la CRDB

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
33m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’