International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Julai 03 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Jul 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Julai 03 2025

West Ham imekataa dau la pauni milioni 50 iliyowasilishwa na Tottenham kumsajili mshambuliaji wa Ghana Mohammed Kudus, 24. (Talksport)

Arsenal ina matumaini ya kumpata mshambuliaji wa Brazil Rodrygo kwa pauni milioni 70. Mchezaji huyo hana uhakika wa kusalia Real Madrid chini ya kocha mpya Xabi Alonso. (Mirror)

Atletico Madrid iko tayari kufanya kila iwezalo kumsajili beki wa Tottenham na Argentina Cristian Romero, 27, na iko tayari kufikia mkataba wa thamani ya takriban Β£61m. (AS - kwa Kihispania)

Sancho yuko tayari kupunguziwa mshahara ili kujiunga na mabingwa hao wa ligi ya Serie A. (Eurosport Italia - kwa Kiitaliano)

Manchester United imepiga hatua katika mbio za kusajili mshambuliaji wa Aston Villa na England Ollie Watkins, 29, na imefanya mazungumzo ya muda na klabu hiyo ya Midlands inayotaka ada ya takriban Β£60m. (Mirror)

Mkufunzi wa Napoli Antonio Conte ana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27, kutoka Atalanta msimu huu wa kiangazi. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Winga wa Japan Kaoru Mitoma, 28, ameiambia Brighton kuwa anataka kusalia katika klabu hiyo na kusaini mkataba mpya licha ya kuhusishwa na kuhamia Bayern Munich (Sky Sports)

Kipa wa Nice Marcin Bulka, 25, anatarajiwa kujiunga na Neom ya Saudi Arabia, licha ya Sunderland kuwasilisha ofa ya pauni milioni 12.8 iliyokubaliwa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland. (Meczyki - kwa Kipolandi)

Mshambulizi wa Italia Ciro Immobile, 35, anatarajiwa kukatisha mkataba wake na klabu ya Uturuki ya Besiktas na kujiunga na Bologna kwa uhamisho wa bila malipo. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Beki wa Valencia Mhispania Cristhian Mosquera, 21, amekataa kandarasi mpya iliyoboreshwa na klabu hiyo ya La Liga kwa sababu anataka kujiunga na Arsenal. (Las Provincias - kwa Kihispania)

Beki wa Wolves Nasser Djiga, 22, huenda akajiunga na Rangers kwa mkopo kwa msimu huu akiwa amecheza mechi tano pekee za Ligi ya Premia tangu Februari. (Express na Star)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’