Local,Normal News,

Samatta afiwa na Baba yake mzazi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
6 Jul 2025
Samatta afiwa na Baba yake mzazi

Mshambuliaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta 'Samagol' amepata msiba mkuubwa wa kufiwa na baba mzazi, Ally Pazi Samatta.

Mzee Samatta amefariki dunia asubuhi ya leo Jumapili akiwa nyumbani kwake Mbagala Dar es Salaam na taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mwanae, Mohamed Samatta.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa familia, Mzee Samatta alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya kwa hivi karibuni.

"Mzee amefariki leo nyumbani hakuwa ameugua kwa muda mrefu na juzi aliniambia njoo mwanangu unione daah! Ndio hivyo tena," amesema mmoja wa ndugu wa karibu wa familia hiyo.

Mzee Samatta enzi za uhai wake alikuwa mshambuliaji nyota aliyewahi kutamba na klabu kadhaa na kuichezea timu ya taifa, akivaa jezi namba 10 na alikuwa mtu mashuhuri katika jamii yake, akiheshimika kwa malezi bora aliyowapatia watoto wake, hasa Mbwana ambaye amekuwa nembo ya soka la Tanzania kimataifa.

Mwenye ez Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, peponi AMEN..

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
5m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
34m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’