Chelsea wana nia ya kumsajili mlinda lango wa Paris St-Germain na Italia Gianluigi Donnarumma, 27. (L'Equipe)
Newcastle wamefufua nia ya kumnunua mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Mfaransa Hugo Ekitike, 23, na wanatumai kuwashinda Liverpool kwenye usajili wake. (Telegraph)
West Ham wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa zamani wa Aston Villa Douglas Luiz kutoka Juventus, huku Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 27 akiwa ametatizika kufanya vyema kwenye Serie A. (Gazzetta dello Sport)
Barcelona wanaendelea kufanyia kazi mikataba ya winga wa Liverpool na Colombia Luis Diaz, 28, na mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 27, lakini hawataharakisha kusajili mchezaji yeyote. (Marca )
Sporting wako tayari kumchukulia hatua za kinidhamu mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 27, baada kutoripoti kwa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya akisubiri kuhamia Arsenal. (Guardian)
Juventus wamewapa Manchester United £8.65m pamoja na marupurupu ili kumtoa winga Muingereza Jadon Sancho, 25. (Sky Sports)
Mchezaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea Aston Villa Emiliano Martinez bado anavutiwa na Manchester United lakini klabu hizo mbili ziko tofauti kabisa na tathmini zao za mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32. (Telegraph)
Arsenal wamepiga hatua katika mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Ethan Nwaneri, 18, kuhusu kandarasi mpya. (Fabrizio Romano)
Newcastle United italazimika kukubali mkataba wa pauni milioni 100 kumsaini mshambuliaji wa Uingereza Ollie Watkins, 29, kutoka Aston Villa msimu huu. (Football Insider)
Mchezaji wa Atletico Madrid Conor Gallagher yuko tayari kurejea katika Ligi ya Premia baada ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza, 25, kutolewa kwa Newcastle. (Team Talk)
Klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal na vilabu nchini Italia vimefanya uchunguzi kuhusu Benjamin Sesko wa RB Leipzig baada ya Arsenal kujitenga na kumsajili mshambuliaji huyo wa Slovenia, 22. (Teamtalk)
West Ham wameiambia Roma kuwa wanataka kumuuza mlinzi wa Morocco Nayef Aguerd, 29, na hawatamruhusu kuondoka kwa mkopo. (Gianluca di Marzio)
BBC



