Simba kusajili kiungo Coastal Union

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th July 2025


Simba kusajili kiungo Coastal Union

Klabu ya Simba inatajwa kuwa katika mchakato wa kumsajili kiungo wa Coastal Union, Hussein Semfuko, imefahamika

Kocha Fadlu Davids amependekeza nyota huyo kuongezwa katika kikosi chake akiamini ataongeza nguvu katika safu yake ya kiungo

Taarifa kutoka chanzo cha karibu na mchezaji huyo, imebainisha mazungumzo yamekamilika na kilichokuwa kinasubiriwa ni kusaini mkataba kusubiri utambulisho rasmi

Simba inaboresha safu yake ya kiungo ambapo mkapa sasa imeachana na viungo watatu Omary Omary, Fabrice Ngoma na Augustine Okejepha


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.