Local,Transfer News,Simba, Azam

Azam Fc yaweka ngumu kwa Fei Toto

Joel JJ By Joel JJ
17 Jul 2025
Azam Fc yaweka ngumu kwa Fei Toto

Saga ya usajili wa kiungo mahiri Feisal Salum ‘Fei Toto’ inaendelea kuchukua sura mpya, baada ya Klabu ya Azam Fc kuweka ngumu juu ya kumwachia nyota wao huyo. Huku Simba ikiendelea kumuwinda, Azam Fc imeweka dau kubwa, likionekana kuziba njia kwa timu zinazotamani huduma ya kiungo huyo fundi.

Kwa mujibu wa taarifa, Fei Toto tayari amefikia makubaliano binafsi na Simba, ambapo Wekundu wa Msimbazi wanamtaka kama chaguo lao la kwanza katika eneo la kiungo cha ushambuliaji, wakitaka kuimarisha safu hiyo kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Hata hivyo, Azam Fc haionekani kutaka kumuachia kirahisi hasa baada ya ujio wa kocha mpya Frolent Ibenge. Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa klabu hiyo, Thabit Zakaria ‘Zakazakazi’, amesisitiza kuwa Fei Toto bado ni mali halali ya Azam, akibainisha kuwa nyota huyo ana mkataba unaoendelea kwa mwaka mmoja zaidi.

“Fei ni mchezaji wetu na bado ana mkataba. Hatuna mpango wa kumuuza. Hata hao wanaomtaka wanajua wazi hali hiyo, ndio maana hawajafanya mazungumzo yoyote rasmi nasi,” alisema Zakazakazi, akipuuzilia mbali tetesi zinazosambaa mitandaoni.

Zakazakazi ameongeza kuwa thamani ya Fei Toto imeongezeka baada ya kujiunga Azam, akisema:

“Thamani anayopata sasa ni matokeo ya muda wake Azam. Timu nyingine walikuwa hawamuoni. Azam tumemjenga kiufundi, tumempa nafasi na sasa ameweza kuonyesha uwezo wake wa kuwaongoza wenzake na kutengeneza ushindi.”

Kwa upande mwingine, taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa juhudi za kuinasa saini ya kiungo huyo bado zinaendelea kwa siri kubwa. Majadiliano baina ya viongozi wa juu wa klabu hizo mbili yanadaiwa kuwa bado hai, huku Simba ikihaha kuhakikisha inampata Fei Toto kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE →
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE →
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE →
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE →
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE →
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE →
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE →