Local,Transfer News,Mashujaa, Simba, Singida

Mgunda azigonganisha Mashujaa Fc, Singida BS

Joel JJ By Joel JJ
28 Jul 2025
Mgunda azigonganisha Mashujaa Fc, Singida BS

Licha ya Mashujaa kumtambulisha aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Ismail Mgunda, kwa ajili ya kukichezea kikosi hicho msimu ujao, kumekuwa na sintofahamu baada ya kudaiwa pia nyota huyo amesaini mkataba na Singida Black Stars.

Nyota huyo aliitumikia Mashujaa msimu wa 2024-25, kisha baadaye kuuzwa kwenda AS Vita Club ya DR Congo katika dirisha dogo la Januari 2025, ingawa, ingawa hakudumu ndani ya kikosi hicho, kwa sababu alikichezea kwa miezi sita tu na kurejea tena nyumbani.

Baada ya nyota huyo kurejea nchini, Mashujaa ikamtangaza kumsajili tena kwa ajili ya kumtumia msimu wa 2025-26, ingawa dili hilo limeingia dosari, kwa kile kinachoelezwa kabla ya kikosi hicho kumtambulisha alishasaini mkataba na Singida. 

“Mchezaji alituambia alivunja mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia na Mashujaa ndio maana wakampa baraka zote za kwenda AS Vita Club, ila tumeshangaa kuona tena wanamtambulisha upya wakati sisi tulimalizana kitambo,” alisema kiongozi mmoja wa Singida.

Chanzo hicho kilisema baada ya Mashujaa kugundua mchezaji huyo amesaini Singida, wakaamua kumtangaza kwa kile wanachodai makubaliano waliyoingia ni endapo atarudi nchini kipaumbele cha kwanza ni cha kujiunga kwao, jambo ambalo halina ukweli.

Mwenyekiti wa Mashujaa Meja Abdul Tika alisema Mgunda ni mchezaji wao halali, japo kumekuwa na timu mbalimbali ambazo zinamshawishi mchezaji huyo ili kujiunga kinyume cha makubaliano waliyoingia hapo mwanzoni. 

“Tunajua kuna klabu zinamshawishi, lakini wakae wakitambua sisi Mgunda ni mchezaji wetu halali na alikuwa amebakisha pia mwaka mmoja, tulimpa ruhusu ya kwenda DR Congo kwa sababu tuliona ni nafasi ya kujitangaza zaidi.” alisema Meja Abdul.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
1h ago
READ MORE →
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
4h ago
READ MORE →
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
6h ago
READ MORE →
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
8h ago
READ MORE →
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: João Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
10h ago
READ MORE →
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
11h ago
READ MORE →
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
11h ago
READ MORE →
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
13h ago
READ MORE →
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
16h ago
READ MORE →
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE →