Klabu ya Simba imemuaga aliyekuwa beki wake Che Malone Fondoh aliyejiunga na USM Algiers
Taarifa ya Simba imebainisha kuwa Che Malone amejiunga na USM Algiers baada ya makubaliano kati ya Simba na waajiri wake hao wapya
Beki huyo raia wa Cameroon alijiunga na Simba Julai 2023 akisaini mkataba wa miaka mitatu ambao ulipaswa kumalizika Juni 2026
Tayari Simba imemtangaza beki wa kati Rushine De Reuck kutoka klabu ya Mamelodi Sundowns kuwa mbadala wake




