Majira ya saa 6 usiku Yanga ilimtambulisha beki wake mpya wa kushoto Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' aliyejiunga na tmu hiyo akitokea klabu ya Simba
Ilikuwa ni suala la muda, Yanga ilifanya 'umafya' kwa watani zao Simba kwa kumnyakua Zimbwe Jr wakati timu hiyo ikipambana kumuongezea mkataba
Zimbwe Jr ameondoka Simba baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka 11, ameshinda mataji yote makubwa akiwa na Simba
Ni rasmi sasa anakwenda kufungua ukurasa mpya kunako klabu ya Yanga
Klabu ya Simba tayari imthibiti mlinzisha kumsajili beki wa kushoto Anthony Mligo kutoka klabu ya Namungo Fc
Mligo ametua Msimbazi kuziba nafasi iliyoachwa na zimbwe Jr




