Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imekuwa timu ya kwanza kutinga robo fainali ya michuano ya CHAN 2024 baada ya kuichapa Madagascar mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mabao ya mapema kipindi cha kwanza yakiwekwa kambani na Clement Mzize yametosha kiuhakikishia Stars ushindi wa tatu mfululizo na kufikisha alama 9
Alifunga bao la kwanza dakika ya 13 akimalizia mpira uliogonga mwamba baada ya shuti la Mudathir Yahya
Mzize alifunga bao la pili dakika ya 20 akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Feisal Salum 'Fei Toto'
Tanzania imejihakikishia kutinga robo fainali ikiwa kinara wa kundi B na alama 9 huku ikiwa na mechi moja ya kukamilisha ratiba dhidi ya Afrika ya Kati

