Manchester City wanafikiria namna ya kuuteka nyara uhamisho wa Chelsea wa kumnunua winga wa RB Leipzig wa Uholanzi Xavi Simons, 22. (Sport)
Brighton watahitaji zaidi ya pauni milioni 100 kwa Carlos Baleba baada ya Manchester United kuonyesha nia ya kumnunua kiungo huyo wa kati wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21. (Telegraph - subscription required)





