Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, Fountain Gate, Singida BS

Stars kazi ni moja dhidi ya Morocco Ijumaa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Aug 2025
Stars kazi ni moja dhidi ya Morocco Ijumaa

Kesho Ijumaa, Agosti 22, macho na masikio ya Watanzania yatakuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo Taifa Stars watakabiliana na Morocco katika robo fainali ya CHAN 2024. Ni zaidi ya mechi ya mpira, ni kipimo cha hadhi ya soka la Tanzania barani Afrika.

Taifa Stars waliweka msingi mzuri hatua ya makundi. Walikusanya pointi 10, wakifunga mabao matano na kuruhusu moja pekee. Safu ya ulinzi imeonekana imara, huku nidhamu ikiwatambulisha kama moja ya timu zilizosalia safi, hakuna kadi nyekundu.

Hii ni sura ya timu inayocheza kwa mpangilio, inalinda matokeo na kuamua pale inapopata nafasi. Ni sababu ya mashabiki wengi kuamini kwamba kesho Stars wana kila kitu cha kusimama imara mbele ya mabingwa wa zamani.

Morocco si wageni kwenye hatua hizi. Wamewahi kutwaa CHAN mara mbili na safari yao mwaka huu imethibitisha ubora wao wa kushambulia. Waliibuka washindi dhidi ya Angola (2-0), Zambia (3-1), na DR Congo (3-1), wakafunga jumla ya mabao manane.

Hata hivyo, walipoteza mchezo muhimu dhidi ya Kenya (1-0), jambo linaloonyesha kuwa wanaweza kushindwa wanapobanwa.
Safu yao ya mbele ni hatari, lakini ukuta wao bado una mashimo, jambo linalowapa Stars tumaini la kupata nafasiΒ 

Unaweza kusema ni mpambano wa falsafa mbili: Stars wakitegemea uimara wa ulinzi na nidhamu, Morocco wakiwa na silaha ya mashambulizi makali.

Faida kwa Tanzania ni kucheza mechi hiyo dimba la Benjamin Mkapa. Mpaka sasa zaidi ya mashabiki 40,000 wana uhakika wa kushuhudia mchezo huo baada ya wadau mbalimbali kununua tiketi. Wanasema shabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani, Stars inawahitaji Watanzania kujaza dimba la Mkapa

Kwa Taifa Stars, huu ni wakati wa kuonyesha dunia kuwa Tanzania si mgeni tena kwenye jukwaa kubwa. Morocco wanakuja na historia ya ubabe, lakini Stars wanaingia na kitu ambacho si rahisi kupewa, imani ya taifa lote.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
9m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
38m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’